Simulizi Nyingi – Simulizi Kutoka Afrika Mashariki

“Hadithi moja hutengeneza kasumba, na tatizo la kasumba sio kwamba ni za uongo, bali ni kwamba hazijakamilika. Zinafanya simulizi moja kuwa simulizi pekee. (…) Simulizi nyingi zinafaa” (Masimulizi ya Ted ya Chimamanda Ngozi Adichie mwaka 2009).

Simulizi nyingi ni jukwaa la kutengeneza mtazamo mwingine wa Afrika na waafrika wenyewe wakielezea simulizi zao wenyewe.

Badala ya kupunguza ukweli wa jamii na watu wa kiafrika kuwa kitu kimoja kidogo kabisa, “simulizi moja”. Chimamanda Ngozi Adichie, mwandishi m-Naijeria, anatuomba katika maongezi yake ya Ted ya mwaka 2009 kusimulia au kuwapa watu nafasi ya kusimulia “simulizi nyingi” kutoka katika mitazamo tofauti, ili kupinga kasumba zisizokamilika. Kama wanahiari wa Kulturweit, tunachangia katika hili kwa kuwapa wa-afrika nafasi ya kusimulia wenyewe katika nchi tunazojitolea: Uganda, Rwanda, Tanzania, Ethiopia na Kenya. Kwa kufanya hivyo, hatutawasilisha kwenu mitazamo yetu wenyewe ila kuwaachia nafasi watu wa nchi hizi kusema simulizi zao wenyewe ili kijukita katika mitazamo yao wenyewe.

“Jinsi simulizi zinavofikishwa kwa jamii, anayezisimulia, wakati zinaposimuliwa, idadi ya simulizi-hutegemea sana nguvu ya simulizi” Chimamanda Ngozi Adichie.

Tunatambua nguvu ya kusimulia na pia kama waandishi wa blogu, bado tunaweza kushawishi uchaguzi wa mada za kuandika.

Zur Werkzeugleiste springen